MAKUMBUSHO

Pia Katika eneo la hifadhi kuna nyumba ya makumbusho iliyoanzishwa kwa ajili yakuhifadhi tamaduni pamoja na historia za makabira mbalimbali ya Tanzania. Ndani ya makumbusho zipo zana za kijadi zilizotumiwa na watu wa kale katika shughuli za vita za makabira, kilimo, uwindaji, uchezaji wa ngoma za asili na upigaji wa lamli. Pia zipo nguo zilizotengenezwa kwa kutumia ngozi za wanyama pamoja na magome ya miti.