Hifadhi ilianzishwa mwaka 2006 chini ya usimamizi wa Mshauri wa kanisa la Uinjilisti mch. Markus Lehner. Katika kipindi hicho wanyama wachache walihifadhiwa katika mapori ya wazi ambapo miongoni mwa wanyama hao ni Pofu, Pundamilia, Nyumbu, Swala pala, Swala grant na Paa.
Wanyama wengine walihifadhiwa kwenye maeneo yenye vizuizi (mabanda) ili kuwapa nafasi wageni kuweza kuwaona kwa ukaribu Zaidi, wanyama hao ni kama vile Kima, Chatu, Mamba, Nungunungu, Abunuasi, Sungura, Fisi, Komba, Kanu, Mbawala, Mbega, Nyoka aina ya mlawe, Bata miiba, Bata Misri, Mbuni, Mwali mweupe, Kanga, Marabou, Kasuku, Tausi pamoja na Flamingo.
Hifadhi ilizinduliwa rasmi mnamo tarehe 18/10/2008 na raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Prof. Jakaya Mlisho Kikwete. Baada ya uzinduzi kufanyika, hifadhi ilifunguliwa na kuanza kutoa huduma.
Hadi kufikia wakati huu, idadi ya wanyama imeongezeka kutokana na kuzaliana ikilinganishwa na kipindi cha nyuma. Hata hivyo jitihada zakuongeza wanyama wengine zinaendelea kufanyika kwa kuzingatia uwezo wa hifadhi.